Joshua 12:5-9

5 aNaye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.

6 bMose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.

7 cHawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:
8
In order to format the table contained in this verse correctly, it has been necessary to move the content of some adjacent verses into it.
,
enchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):

 9 fmfalme wa Yeriko mmoja
mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja
 10 gmfalme wa Yerusalemu mmoja
mfalme wa Hebroni mmoja
 11 hmfalme wa Yarmuthi mmoja
mfalme wa Lakishi mmoja
 12 imfalme wa Egloni mmoja
mfalme wa Gezeri mmoja
 13mfalme wa Debiri mmoja
mfalme wa Gederi mmoja
 14 jmfalme wa Horma mmoja
mfalme wa Aradi mmoja
 15 kmfalme wa Libna mmoja
mfalme wa Adulamu mmoja
 16 lmfalme wa Makeda mmoja
mfalme wa Betheli mmoja
 17 mmfalme wa Tapua mmoja
mfalme wa Heferi mmoja
 18 nmfalme wa Afeki mmoja
mfalme wa Lasharoni mmoja
 19 omfalme wa Madoni mmoja
mfalme wa Hazori mmoja
 20 pmfalme wa Shimron-Meroni mmoja
mfalme wa Akishafu mmoja
 21 qmfalme wa Taanaki mmoja
mfalme wa Megido mmoja
 22 rmfalme wa Kedeshi mmoja
mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja
 23 smfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori)
Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori.
mmoja
mfalme wa Goimu katika Gilgali mmoja
 24 umfalme wa Tirsa mmoja

wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.

Copyright information for SwhNEN